×

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Amuwakilisha Rais Samia Kumjulia Hali Edward Lowassa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Mama Regina Lowassa, mke wa Waziri Mkuu Mstaafu (wa tatu kushoto) na Fredrick Lowassa (kulia) alipokwenda kumjulia hali Edward Lowassa anayepatiwa matibabu jijini Johannesburg, Afrika ya Kusini

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwakilisha Dkt. Samia Suluhu Hassan kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa anayeendelea na matibabu Afrika ya Kusini.

Akizungumza na wanafamilia kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Samia, Waziri Mkuu amewasilisha salaam za pole kutoka kwa Mheshimiwa Rais na kusema Mheshimiwa Rais anafuatilia hali ya Mheshimiwa Lowassa kwa ukaribu na anamuombea afya njema.

Waziri Mkuu ametoa salamu hizo Jumatano, Desemba 28, 2022 jijini Johannesburg, Afrika Kusini ambako alienda kumjulia hali  Lowassa.

Kwa upande wake, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Regina Lowassa amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa jinsi ambavyo amekuwa karibu na wanafamilia na namna ambavyo anafuatilia matibabu ya mpendwa wao.

Naye mtoto mkubwa wa Mheshimiwa Lowassa na Mbunge wa Monduli, Bw. Fredrick Lowassa amewashukuru Watanzania kwa maombi yao ya kumtakia afya njema baba yao.

Leave a Comment