
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameuagiza wakala wa barabara Tanzania TANROADS kuhakikisha ndani ya mwaka mmoja michakato yote ya ujenzi wa barabara kutoka Wilayani Malinyi Mkoani Morogoro hadi Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma unakamilika ili kufungua mawasiliano ya wananchi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Itete mara baada ya kuwasili wilayani Malinyi kutokea wilayani Kilombero Chongolo amesema kuwa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 48 kutoka Malinyi mpaka namtumbo ujenzi wake utaunganishwa na barabara ya Kidatu Ifakara.

Aidha Katibu Mkuu huyo ameeleza barabara hiyo inakadiliwa kutumia gharama ya kiasi cha Shilingi Bilioni 200 ambayo mpaka sasa TANROADS wameshatangaza zabuni yake.