
Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Nchini (CMSA), kwa kushirikiana na Taasisi ya Charted Institute for Security and Investment (CISI) ya nchini Uingereza, wanatarajiwa kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa masoko ikiwa ni pamoja na madalali wa masoko ya hisa, wachuuzi, wawakilishi wao, washauri wa uwekezaji, wahasibu na kadhalika.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kuchukua muda wa wiki sita, kuanziaApril 17, 2023 hadi Mei 31, 2023 ambapo yatakuwa yakiendeshwa nyakati za jioni ili kuwapa nafasi wadau wengi zaidi kushiriki na baada ya mafunzo kumalizika, washiriki watafanya mtihani na kupewa leseni.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa CMSA, imeeleza kuwa mafunzo hayo yatakuwa yakitolewa katika Ofisi za CMSA zilizopo Mtaa wa Garden, Posta jijini Dar es Salaam.
