
Dar es Salaam 11 Februari 2023: Kampuni ya Shafa Mills inayojishughulisha na kilimo na ufugaji imedhamiria kuikomboa sekta ya ufugaji hapa nchini kwa kuzalisha chakula bora cha mifugo kama ng’ombe na vifaranga ili wafugaji waweze kufaidika na mifugo yao.
Kampuni hiyo ambayo kwasasa imeingia sokoni na bidhaa yake ya Shafa Farm Dairy Milk ambayo ni maziwa halisi ya ng’ombe kutoka shambani kwao mkoani Iringa moja kwa moja na kuwafikia wateja imekuwa wazalishaji wakubwa wa bidhaa hiyo hapa nchini.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar, kwenye semina iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwaajili ya kuwapa ujuzi wafugaji, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Mohammed Nasri amesema lengo lao ni kuwanufaisha wakulima na wafugaji hapa nchini.
Mkurugenzi huyo amesema hapo awali walipoanzisha shamba lao la ufugaji mkoani Iringa mwaka 2019 walikumbana na changamoto nyingi za kupata chakula bora kwa ajili ya mifugo yao ili waweze kupata mifugo yenye afya njema ndipo wakaanzisha Shafa Agro ambayo ni idara inayojishughulisha na maziwa na utengenezaji wa chakula cha mifugo.

Mkurugenzi huyo amesema kwa kutumia chakula hicho sasa wanamifugo yenye bora na kuwafanya ng’ombe wao kutoa maziwa kwa wingi ambapo ng’ombe mmoja amekuwa na uwezo wa kutoa mpaka lita 30 kwa siku.
Katika semina hiyo kampuni hiyo imezindua chakula bora cha mifugo kama ng’ombe na mbuzi wa maziwa kuwa na afya bora na kutoa maziwa kwa wingi pia wamezindua chakula bora cha viranga na kuwafanya wakue kwa haraka na kuwa na afya bora ili kumnufaisha mfugaji.

Mkurugenzi huyo amewataka wafugaji kutumia vyakula vya kampuni hiyo kwa ajili ya kupata zao bora na faida kubwa ambapo sasa vinapatikana kwenye maduka ya vyakula vya mifugo.