×

Yanga Yavunja Ukimya Ishu ya Feisal Salum ‘Fei Toto’ Kuonekana Dimba la Mkapa, Dar

UONGOZI wa Yanga umevunja ukimya na kuweka wazi kuwa suala la kiungo wa timu hiyo, Feisal Salum ‘Fei Toto’ litajulikana kwenye mchezo wao dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo, kesho Jumapili kwenye Dimba la Mkapa, Dar.

Ikumbukwe kiungo huyo alitangaza  kuvunja mkataba  wake na timu hiyo  kwa kulipa kiasi cha Sh milioni 112 kabla ya kufungua shauri katika Kamati ya  Sheria na Hadhi za Wachezaji  ya Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ ambalo liweka wazi kuwa kiungo bado ni mchezaji wa timu hiyo na mkataba wake unamalizika 2024.

Kamwe ametoa kauli hiyo kufuatia tetesi za uongozi wa timu hiyo kumalizana kwa kuingia mkataba mpya na kiungo huyo baada ya baadhi ya vigogo wa serikalini kuingilia kati kuweza kulimaliza suala hilo.

Taarifa za ndani kutoka ndani ya kutoka ndani ya timu hiyo zinadai kuwa kiungo huyo amekubali kurejea kwa mkataba wa miaka miwili huku dau lake likiwa ni sh milioni 350 na mshahara wa sh 15 kwa mwezi.

Akizungumza na Championi Ijumaa, kuhusiana na ishu ya Feisal ilipofikika, Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe alisema kuwa, suala la kiungo wao huyo lipo vizuri na Jumapili atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaokuwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa wakati Yanga ikiwavaa TP Mazembe kuanzia saa 1:00 usiku.

“Fei Toto ni mchezaji halali wa Yanga, suala la yupo kambini au hayupo ni Jumapili tutakapocheza dhidi ya TP Mazembe, atakuwa sehemu ya wachezaji wote uwanjani,” alisema Kamwe huku akiwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuisapoti timu yao.

Stori Na Ibrahim Mussa

Leave a Comment