×

Viongozi wa Afrika wanakutana Addis Ababa Kwenye Mkutano wa 36 Umoja wa Afrika (AU)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu akizungumza kwenye Mkutano wa 36 Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika katika Ukumbi wa Nelson Mandela uliopo Makao Makuu ya Umoja huo Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 18 Februari, 2023.

Wakuu wa nchi za Afrika wameanza mkutano wao wa kila mwaka katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Mkutano wa mwaka huu wa Umoja wa Afrika unafanyika huku kukiwa na ongezeko la ukosefu wa usalama katika baadhi ya maeneo ya bara hilo na mzozo mkubwa wa chakula huku nchi kadhaa zikikabiliwa na ukame mkali.

Huu ni mkusanyiko wa kwanza mkubwa wa viongozi kutoka barani kote Addis Ababa tangu AU ianzishe makubaliano ya amani kati ya serikali ya Ethiopia na vikosi vya eneo la Tigray nchini humo.Mkataba huo ulihitimisha moja ya mizozo mibaya zaidi ya kivita barani Afrika.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa 36 Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika katika Ukumbi wa Nelson Mandela uliopo Makao Makuu ya Umoja huo Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 18 Februari, 2023.

Kufuatia makubaliano hayo mapigano yamesimama na upatikanaji wa misaada ya kibinadamu umeongezeka.

Sasa AU inapaswa kushughulikia matatizo ya kiusalama kutoka eneo la Sahel huko Afrika Magharibi hadi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wakati huo huo mamilioni wanakabiliwa na njaa katika Pembe ya Afrika kutokana na ukame mkali zaidi katika vizazi viwili.

Mkutano huo wa kilele wa siku mbili pia unatarajiwa kutoa wito wa kuongezwa nguvu katika utekelezaji wa mpango wa biashara huria barani kote

Leave a Comment