×

Benki Absa Yaboresha Mkopo wa Nyumba, Yaingia Makubaliano na NHC

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula (katikati) akipokewa na, kutoka kushoto;  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Mchechu, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa, Ndabu Lilian Swere na Mkurugenzi Mtendaji wa Absa Tanzania, Abdi Mohamed wakati akiwasili katika jengo la Morocco Square

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula amefika katika jengo la Morocco Square kuzindua Huduma ya Mkopo wa nyumba ulioboreshwa wa benki ya Absa sambamba na utiaji saini hati ya makubaliano yanayowezesha wateja wa Benki ya Absa kununua nyumba za Shiirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa mkopo. Hafla ambayo ilifanyika jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula (katikati) Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Mchechu (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed (kushoto) wakionyesha mfano wa hati  ya makubaliano muda mfupi mara baada ya kuisaini ili kuwezesha wateja wa Absa  kununua nyumba za NHC kwa mkopo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula (kushoto) akishikana mikono na  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed, katika hafla ya uzinduzi wa Huduma ya Mkopo wa nyumba ulioboreshwa wa Absa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Anayeangalia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula (katikati) Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Mchechu (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed (kushoto) wakipozi kwa picha ya kumbukumbu na baadhi ya maofisa wa Absa na NHC mara baada ya hafla ya uzinduzi wa Huduma ya Mkopo wa nyumba ulioboreshwa wa Absa

Leave a Comment