×

Waziri Aweso Atua London Kwenye Mkutano Maalum wa Maji Duniani

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amefika London Uingereza na kuanza kwa kusaini kitabu cha wageni na kutoa salam katika makazi ya Mhe Balozi wa Tanzania Uingereza Dkt.Asha-Rose Migiro ikiwa ni pamoja na kuzungumza na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania Uingereza.

Waziri Aweso akiambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga wamewasili London kwa Mkutano maalum unaohusiana na sekta ya Maji Duniani wa World Water Innovation Summit (WWIS) 2023.

Kupitia Mkutano huu unaohusisha wadau wa sekta ya Maji duniani viongozi na wataalamu watajadili changamoto kubwa zinazoikabili mifumo ya usambazaji maji na usafi wa mazingira (majitaka).

Aidha, Mkutano huu unatarajiwa kuwa na mjadala wenye kutoa suluhu ya pamoja ya namna bora ya kuboresha mifumo ya usambazaji Majisafi na usafi wa mazingira nchini (Majitaka) hususani katika utekelezaji wa Miradi mikubwa ikiwemo ya mabwawa inayoendelea na inayotarajiwa kujengwa nchini kwa kuzingatia mabadiliko ya Tabia nchi.

Leave a Comment