×

Simba Yaandaa Nondo Mpya Kimataifa Mwenyekiti wa Bodi Afunguka

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’.

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ ameweka wazi kuwa, kwenye mechi za kimataifa zitakazofuata ambazo watacheza Uwanja wa Mkapa, watapambana kufanya jambo la tofauti.

Simba katika mchezo wa kwanza Kundi C kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu waliocheza nyumbani, ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 0-3 Raja Casablanca.

Mchezo ujao nyumbani ni Machi 8, mwaka huu ambapo Simba inatarajiwa kucheza dhidi ya Vipers ya Uganda, kumbuka Jumamosi iliyopita wakiwa ugenini, Simba waliifunga timu hiyo bao 0-1.

Ikimalizana na Vipers, itacheza tena nyumbani dhidi ya Horoya AC, Simba inakumbuka ilipoenda Guinea, ilifungwa bao 1-0 na Horoya, hivyo inataka kulipa kisasi.

Kikosi cha Simba.

Try Again amesema wanatambua walifanya makosa kwenye mchezo dhidi ya Raja Casablanca, lakini kwa mechi zijazo hawatafanya makosa.

“Tulipoteza mchezo wa kwanza tukiwa nyumbani, hakuna ambaye alitarajia, lakini kwa mchezo ujao dhidi ya Vipers tunaamini tutapata matokeo mazuri ya ushindi.

“Kwenye mechi za kimataifa kila timu inapambana kupata matokeo mazuri ikiwa nyumbani na ugenini, na sisi pia tunahitaji matokeo mazuri nyumbani na ugenini, Watanzania wazidi kutuombea.

“Mbali na Vipers, pia tuna mchezo dhidi ya Horoya nyumbani, unaona nao pia ni mchezo muhimu kwetu, lazima tufanye kweli na tuzidi kuwa kwenye mshikamano mkubwa,” alisema Try Again.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA

MZEE ALIYEMILIKI NYUMBA 5 ANALALA KWENYE KONTENA MIAKA 7, ADAI KUVUNJIWA NYUMBA ZAKE KIHUNI…

Leave a Comment