
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Adamu Malima amemwagia sifa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa Mwita Waryoba kwa kuisimamia vyema Halmashauri ya Buchosa.
Kauli hiyo aliitoa wakati wa zaiara yake ya kukagua miradi ya mendeleo kwenye Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza.

“Tumekuleta Buchosa kwa kazi moja tu kusimamia mapato na kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo ilikuwa imekwama kutokana na usimamizi mbovu uliokuwepo,
Kwa kipindi kifupi hiki toka uhamie Buchosa tunaona matunda yako kazi nzuri ya kusimamia mapato ya Halmashauri tunahitaji upeleke pesa kwenye miradi ili ikamilike kwa wakati na wananchi waweze kuitumia na ndio kitu anahitaji mhe. Rais Samia Suluhu Hassan” Malima.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa Mwita Waryoba amesema wakati anakàbidhiwa jukumu la kuiongoza Halmashauri ya Buchosa alikuta wanakusanya Sh.20milioni kwa wiki alipoanza usimamizi mzuri na kuweka mikaka na mipango mizuri ya kusimamia na ukusanyaji wa mapato kwa sasa wanakusanya Sh.84milioni kwa wiki hii nihatua kubwa nitaendelea kupambana hadi nifike makusanyo ya Sh.100 milioni kwa wiki.
” Nimeweka mikakati kila mkuu wa idara asimamie idara yake na ahakikishe anawasimamia watu wake wakusanye mapato na siyo vinginevyo lengo la ukusanyaji wa mapato nikusaidia kukamilisha miradi ya maendeleo ya wananchi ili iweze kukamilika na waanze kuitumia, amesema Mwita.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Buchosa Idama Kibanzi amesema Serikali haijakosea kumuleta Mwita Waryoba kukaimu nafasi ya ukurungezi kwenye Halmashauri ya Buchosa kwa kipindi hiki kifupi alichofika na kuanza kazaa matunda yake tunayaona na hakika Halmashauri yetu itasonga mbele.
” Huyu ni mtu sahihi kwa Halmashauri yetu utendaji kazi wake unaonekana anania ya dhati ya kuitumikia serikali na wananchi wa Buchosa kwa niaba ya Baraza la Madiwani Buchosa tutampatia ushirikiano wa kutosha wakati anatekeleza majuku yake , amesema Kibanzi.

Kwa upande wake Mbunge wa Buchosa Eric Shigongo amesema mkurugenzi wa Buchosa Mwita Waryoba ajikite kusimamia ukusanyaji wa Mapato kwani wananchi wanataka matokeo ya Serikali, ameaminiwa kusimamia jukumu hilo anapaswa kufanya kazi kwa bidii na kuhakisha Halmashauri inasonga mbele.
“Anatakiwa kuchapa kazi matokeo ndiyo msingi wa kipimo cha Kiongozi yoyote, nitashirikiana naye kwa kila jambo ili Buchosa isonge mbele, amesema Shigongo.
Stori na Idi Mumba/Mwanza