×

Chama cha soka Simiyu wafanya maboresho ya katiba

Chama cha soka mkoa wa Simiyu (SIFA) March 4 mwaka huu  kilifanya mkutano mkuu wa kawaida ambapo pamoja na mambo mengine chama hicho cha soka kilifanya marekebisho ya katiba yake ili iendane na ile ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) ambapo kwa kauli moja baada ya mkutano huo wajumbe walimteua Yohana Sitta kuwa katibu mkuu wa kuajiriwa wa chama hicho  baada ya maboresho hayo ya katiba.

Mwenyekiti wa chama hicho Osuri Kossuri ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka hapa nchini TFF amesema “Tulikua na mkutano wetu mkuu wa kawaida ambapo lengo ilikua ni kufanya maboresho na mabadiliko ya katiba yetu ili iendane na ile ya TFF”

“Katiba yetu ya mwanzo ilikua inatoa fursa kila wilaya kuleta wajumbe wanne kwenye mkutano mkuu, na kwa sasa baada ya mabadiliko kila wilaya itaweza kuleta wajumbe wawili tu na maelekezo haya yametoka FIFA ambapo dhumuni ni zile fedha ambazo zingetumika katika kupeana posho baada ya kikao zitumike kuendeleza soka katika mkoa wetu”

“Mbali na wajumbe pia katiba yetu ya sasa ambayo imefanyiwa maboresho ni kwamba nafasi ya Katibu mkuu itakuwa ya kuajiriwa na tayari tulimteua Yohana Sitta kuwa Katibu mkuu wetu ambapo atakuwa akifanya kazi na sekretarieti na mabadiliko haya yalianzia TFF ambapo kila mwanachama wake lazima ayafuate lengo kuu ni kuona watendaji wachache wanaweza kuhakikisha maendeleo ya soka yanapatikana tofauti na hali ilivyokuwa huko nyuma”

Leave a Comment