
Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ameelekeza kuundwa kwa mfuko wa fidia kwa uharibifu unaofanywa na wanyamapori katika vijiji vyao ili waathirika wa uharibifu huo walipwe stahiki zao mapema.

Chongolo ameeleza hayo leo Machi 9, 2023 katika kijiji cha Ndaleta kilichopo wilayani Kiteto baada ya kupokea malalamiko ya wananchi kuhusu uharibifu unaofanywa na tembo kutoka hifadhi ya Taifa ya Tarangire wanaovamia mashamba yao.
Akiwa katika kijiji hicho, wananchi wamelalamikia kuvamiwa na tembo ambao wanaharibu mazao yao mashambani, jambo ambalo linawafanya wakose chakula na kutolipwa fidia zao kwa uharibifu huo.