×

Wanawake Wa Kampuni Ya Bima Ya Strategis Waacha Alama Ya Kipekee Katika Hospitali Ya Mwananyamala

Meneja Masoko wa Strategis Insurance, Lilian Malakasuka, (kulia) akikabidhi kwa Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala, Lilian Karibumackinhtosh za kutandika katika magodoro ya kina mama wakati wakujifugua ikiwa ni sehemu ya misaada iliyotolewa kwa wanawake katika wodi ya wazazi hospitalini hapo na wafayakazi wanawake wa Strategis Insurance ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

WAFANYAKAZI wanawake wa kampuni ya bima ya Strategis wameacha alama ya aina yake kwa akina mama katika wodi ya wazazi ya Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala baada ya kuadhimisha siku hiyo kwa kwenda kusherehekea siku hiyo adhimu na wakina mama waliyopo katika wodi ya wazazi ya Hospitali hiyo Siku ya tarehe 08.03.2023

Wafayakazi hao walitoa zawadi mbalimbali yakiwemo mahitaji muhimu kwa mama na mtoto na kupata  muda wa kubadilishana mawazo na wanufaika hao huku wakiwapa matumaini.

Meneja Masoko wa Strategis Insurance, Lilian Malakasuka, (kulia) akikabidhi kwa mmoja wa viongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala, Lydia Nzema misaada ya sabuni za kufulia, diaper na wipes za watoto,kamamahitaji muhimu kwa mama na mtoto, vifaa hivyo viliyotolewa kwa wanawake katika wodi ya wazazi hospitalini hapo na wafayakazi wanawake wa Strategis Insurance ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambazo zilifanyika jana tarehe 8 March,2023.

Hii ni mara ya pili mfululizo kwa wanawake wa kampuni ya bima ya Strategis kutoa msaada na mahitaji ya aina hii katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani.

“Tunayo furaha mno kujumuika leo hapa kuwasaidia wanawake wezetu hususani katika sikukuu hii ya Wanawake Duniani. Tumewaletea zawadi mbalimbali ambazo zitasaidia wakina mama kabla na baada ya kujifugua,” alisema Meneja Masoko wa kampuni ya bima ya Stategis, Ms. Lilian Lema Malakasuka.

Misaada iliyotolewa kwa wanawake katika wodi ya wazazi hospitalini hapo na wafayakazi wanawake wa Strategis Insurance ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Alisema msaada huo ulijumuisha, sabuni za kufulia, pampers na wipes kwaajili ya Watoto waliozaliwa na hata waliolazwa hapo hospitalini, pamoja na mackintosh maaluum za kutandika kwenye magodoro ya kina mama na Watoto wawapo wodini.

Wafanyakazi wanawake wa Strategis Insurance wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kukabidhi misaada hiyo.

“Vitu hivi ni muhimu sana kwa matumizi ya mama na mtoto hasa wakati wakinamama wanapotoka kujifungua na wawapo wodini na kwa kuzingatia kuwa sio wakina mama wote wenye uwezo wa kununua, wanawake wa kampuni ya bima ya Strategis waliamua kuja kutoa msaada tukiamini vifaa hivi vitaziba pengo kubwa lililokuwepo,” alisema na kuogeza kuwa, hii ni mara yao ya pili mfulululizo wakitoa mahitaji haya muhimu hapa Hospitali ya Mwanayamala na wataedelea kufanya hivi kila mwaka.

Wafanyakazi wanawake wa Strategis Insurance na baadhi ya wahudumu wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala wakati wa kukabidhi misaada hiyo.

Alitoa wito kwa mashirika mengine na wanawake kote nchini kuwakumbuka watu wenye mahitaji maalum hasa wanawake na Watoto ambao ni watu muhimu katika jamii.

Hii ni siku yetu kwa hivyo lazima tuendelee kuonesha umuhimu wa mwanamke katika jamii na pia tuedelee kujiami kila mara.

Wanufaika wa msaada huo hawakuficha furaha yao huku wengi wao wakiimba na kucheza kwa furaha. Waliwapongeza wanawake wa kampuni ya bima ya Strategis kwa kuwakumbuka.

Kwa upande wake, Katibu wa hospitali hiyo, Lilian Mwanga aliishukuru kampuni ya bima ya Strategis kwa muendelezo wake wa kusaidia Hospitali ya Mwananyala hususan kina mama walioko katika wodi ya wazazi, kwani wao ni watu muhimu katika kuleta viumbe vipya duniani.

Alitoa wito kwa kampuni hiyo pia kuagalia namna ya kutoa msaada kwa maeneo mengine ya Hospitali hiyo ili kuwawezesha watoe huduma kwa kiwango cha juu zaidi.

Leave a Comment