PASS Trust yahimiza kilimo chenye tija katika mazingira kwenye warsha ya ukuaji wa uchumi wa kijani shirikishi iliyofanyika Kanda ya Magharibi, na Kaskazini Mikoa ya Tabora, Kilimanjaro-Moshi.
Katika warsha hiyo Taasisi ya PASS Trust imezungumza na wadau mbali mbali waliopo katika mnyororo wa wa kilimo katika mikoa hiyo na kuwahimiza kufanya uzalishaji unaofuata misingi ya ukuaji wa kijani shirikishi.
Warsha iliyofanyika mkoani Tabora ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Mheshimiwa Zacharia Mwansusa ambaye alisema kampeni ya KIJANISHA MAISHA chini ya Taasisi ya PASS Trust itasaidia Mkoa wa Tabora katika kutunza misitu na mazingira ambayo kwa miaka ya karibuni yameharibika kutokana na uharibifu unaotokana na shughuli za kibinadamu.
#kijanishamaisha #passtrust #passkilimo #passtanzania #kilimo Yafuatayo ni matukio mbalimbali katika warsha hiyo
