×

Safiri Bure na Chapride Kwenda Uwanja wa Taifa Kuishuhudia Taifa Stars Ikimenyana na Uganda Leo

Kampuni ya Chapride Tanzania ambayo ni ya usafirishaji abiria na huduma nyingine kwa njia ya mtandao, leo imetoa ofa kwa mashabiki watakaokwenda kuishangilia Timu ya Taifa ya Tanzania, kusafiri bure.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Masoko wa Chapride, Zakayo Shushu, alisema:

“Kwa mwenywe mpango wa kwenda Uwanja wa Mkapa kuishangilia Taifa Stars ikicheza na Uganda akitumia usafiri wa Chapride atafuatwa alipo na kupelekwa uwanjani, atapaswa kumlipa dereva kama kawaida na Chapride itamrudishia pesa kikamilifu na malipo siku ya pili baada ya kupitia taarifa kwa ukamilifu.

Hii ni njia ya kuunga mkono jitihada za Serikali.”

Ikiwa bado hujajiunga na huduma hii, pakua App ya Chapride kupitia Playstore au Appstore.

Leave a Comment