×

Elimu ya Kijinsia Katika Jamii Ni Muhimu Katika Kudhibiti Matukio ya Ukatili

Jinsia ni mtazamo ambao umejengeka katika jamii unaotofautisha majukumu, majukumu hayo na mitazamo hiyo hutengenezwa na jamii husika na mitazamo hiyo inakua haina uhalisia ndani yake.

Ni muhimu kuwa na malezi mazuri ya kijinsia yatakayolenga kuwasaidia watoto kukabiliana vyema na hali yao ya kuwa wavulana au wasichana ili jinsia iwajenge badala ya kuwabomoa.

Ukosefu wa elimu ya jinsia katika jamii hupelekea migogoro ya kiafya inayopelekea msongo wa mawazo kupita kiasi.

Kwa mujibu wa Zuhura Mbinga, ambae ni mtaalamu wa mambo ya kijinsia anaeleza kua, elimu ya jinsia ni namna jinsia mbili zinavyopewa ujuzi ilikujitambua ni jinsi gani ya kuishi katika misingi ya haki na usawa.

Kunaviashiria mbalimbali vinavyo onyesha kua kuna ukosefu wa elimu ya jinsia katika jamii miongoni mwa viashiria hivo ni migogoro inayojitokeza katika jamii baina ya jinsia mbili haswa kwa wale wanandoa, kiashiria kingine ni cha ukosefu wa elimu ya kijinsia na wingi wa kesi na matukio yanayo ripotiwa na mamlaka husika.

Ili kuwa na jamii yenye elimu ya kijinsia hatunabudi kua na njia ya kuwafundisha Watoto wadogo mashuleni kuanzia katika ngazi ya shule ya msingi juu ya suala zima la elimu ya jinsia ili waweze kujua namna ya kuishi na jinsia engine.

 

Elimu hii ya kijinsia pia itasaidia katika ufundishaji wa malezi ya Watoto wa jinsia tofauti, wenye uwezo sawa wa kujitambua na kutanua uwezo wao katika jamii ya kisasa.

Katika utoaji wa elimu hii ya kijinsia ni muhumi jamii kutambua kua huduma za kiakimiliki na kibaiolojia ni mahitaji tu uwezekano wa tofauti za kiakili kati ya wavulana na wasichana.

Tofauti hizi za akili huundwa chini ya ushawishi wa sababu za kijamii ikiwapo mazingira ya kijamii na malezi kama matokeo, tuna nafasi ya kuzingatia masuala ya kulea wasichana na wavulana sio kama aliyopewa tangu kuzaliwa.

Katika jamii ya sasa kuna uhitaji wa msichana kuwa na dhamira, mpango, uwezo wa kutetea maslahi yao na kupata matokeo na si yule tu ambaye anaweza kuonyesha sifa za jadi za kike kama vile upole, uanamke, mtazamo wa kujali kwa wengine.

Ni ngumu kutaja sifa za kiume sababu kwa wanaume ukweli utahitajika kutoka kwao uvumilivu, usikivu, unaweza kuwaokoa.

Katika kipindi hiki cha utoto wa shule ya mapema ndipo mtoto huitaji sifa zote muhimu Zaidi, kwani mielekeo na uwezo huundwa katika umri huu.

Utambuzi wa kijinsia wa Watoto hufanyika tayari katika umri wa miaka mitatu au minne ambayo ni mwisho wa umri mdogo, mtoto hujihusisha na jinsia yake ingawa bado hajajua ni dhana gani za mwanamume na mwanamke inapaswa kujazwa mifano ya tabia ya kiume na ya kike huingia saikolojia ya mtoto kupitia uchunguzi wa moja kwa moja wa tabia ya wanaume na wanawake.

Kwa majibu wa shirika la elimu, sayansi na utamaduni (UNESCO),wasichana wengi Zaidi wako shule hii leo kuliko wakati mwingine wowote, lakini sababu za kijamii,kiuchumi na ubaguzi wa kijinsia zinawazuia wasichana hao kupata fursa sawa ya kumaliza na kufaidika na elimu waliyo chagua.

Shirika hilo linasema hofu kubwa ni ushiriki mdogo wa wasichana katika masomo ya sayansi, teknolojia, uhandishi na hisabati (STEM) na ajira katika nyanja hizo.

 

UNESCO inasema STEM inatamalaki katika kila nyanja ya maisha na ni kuchocheo cha kufikia malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG hapo 2030, na ya pia kutatua changamoto zilizopo na zinazoibuka.

Sasa UNESCO inalivalia njuga suala hilo kwa kulahisisha uelewa na umuhimu wa STEM kwa wasichana na kushughulikia sababu zinazoathiri ushiriki wao.

 

Abdul Juma ambae ni mzazi mwenye Watoto wawili mkazi wa Mikocheni anasema kua elimu ya jinsia inaumuhimu mkubwa sana katika jamii yetu ya sasa kwa Watoto na watu wazima kwani matukio ya kinyanyasaji yanatokana na ukosefu wa elimu ya kijinsia katika jamii zetu.

Jamii yetu haina budi kufikishiwa elimu ya kijinsia ilikuepukana na matukio hayo ya kijinsia haswa kwa Watoto ambao wanaiga kila aina ya tabia ambayo inafaida kwa wengine na tabia mbaya za watu wazima, ambazo nitabia mbaya za kijamii zinazo pelekea kua na kizazi kisicho kuwa na ujuzi wa mambo ya kijinsia.

Hivyo sisi wazazi hatuna budi kuchukua jukumu la kuwalea Watoto katika misingi mizuri ilikuepukana na unyanyasaji wa kijnsia katika jamii zetu.Kwa ushirikiano wa wazazi na walimu mashuleni kuwafundisha watoto itasadia kubadilisha mitazamo ya wanajamii kuhusu usawa wa kijinsia.

Katika chapisho la Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA)2017. Lililokuwa linahusu Ukatili wa kijinsia na athari zake, (Ukurasa wa 27) linasema, kumpiga mwanamke ni unyanyasaji na udhalilishaji, Kipigo husababisha chuki, woga, visasi na uhusiano mbaya ndani ya famili.

Mwanaume wa kweli hawezi kumpiga mwanamke, mwanamke jasiri hutoa taarifa kuhusu vipigo.

Pia katika (ukurasa wa 42) unasema jamii nyingi hazijapata elimu kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia. Hivyo viongozi wanajamii na waragabishi wanawajibu mkubwa wa kuielimisha jamii kuhusu sababu aina na athari za ukatili wa kijinsia.

Wanufaika wa elimu hii wanao mchango mkubwa katika kubadilisha mtazamo na matendo ya wanajamii wengi. Kwa ushirikiano huo tunaweza badilisha mitazamo ya wanajamii kuhusu usawa wa kijinsia.

Utafiti uliofanywa na shirika la (TDHS) unaonyesha kuwa kwenye kila wanawake kumi wanawake watatu wamewahi kufanyiwa vitendo vya ukatili. Na kwamba wanawake wanne kati ya kumi wamewahi kukumbana na ukatili wa kimwili tangu wakiwa na umri wa miaka kumi na tano.

Pia kwa mujibu wa shirika hili la TDHS linasema asilimia 58 ya wanawake na 40 ya wanawake wanakubali kwamba ni sahihi mume kumpiga mke wake kwa sababu mbalimbali.

Kwa mujibu wa shirika la (TN Doronova,2008) linasema kua ni muhimu na itapendeza kuwashirikisha wazazi katika mchakato wa elimu ya jinsia katika mfumo wa mwingiliano kati ya familia na taasisi ya elimu ya mapema.

Rose Mbaga ambae ni mhadhiri wa mambo ya kijinsia anasema si tu elimu inayotolewa shuleni juu ya masuala ya kijinsia inaweza kwqsababu ya kujenga jamii isiyokua na matukio ya kinyanyasaji bali hata mazingira ni moja wapo ya njia ya kujenga jamii yenye utu, ubinadamu kwa watu wazima na hata watoto na kua kama chanzo cha ujuzi wao wa kibinafsi na uzoefu wa kijamii.

Mazingira sio tu hutoa aina tofauti za shughuli kwa watoto wa shule za msingi lakini pia hufanya msingi wa shughuli zake za kujitegemea, kwa kuzingatia sifa za kijinsia.

Katika hali hii kama mtu mzima huna budi ya kua na jukumu la kufungua kwa jinsia zote anuwai yote ya uwezekano wa mazingira na kuelekeza juhudi zao za kutumia vitu vya binafsi,ikizingztia jinsia na tabia za kibinafsi na mahitaji ya kila mtoto.

“Ili kuepukana na jamii yenye matukio ya unyanyasaji wa kijinsia na kua na jamii yenye ufahamu kuhusu masuala ya kijinsia hatuna budi kuelimisha jamii nzima kwa kuandaa vipindi au mafunzo kwa wanajamii wote na kukemea mila na tamaduni zilizo zoeleka katika kila jamii juu ya masuala ya kijinsia haswa katika mgawanyo wa kazi na majukumu baina ya jinsia zote mbili.

Hii itasaidia kua na wanajamii wenye kujiamini na kujitambua na kufanya vitu kwa ujasiri haswa wanawake, pia itasadia kuepukana na migogoro haswa katika ndoa na katika mgawanyo wa mali, pia itasaidia kuleta mtazamo tofauti baina ya wanajamii juu ya maswala ya kijinsia ambayo itapelekea kua na jamii yenye usawa na haki kwa jinsia zote mbili”. Mhadhiri Mbaga anaeleza.

Maira Kunyaranyara ambaye ni mwanasosholojia anaeleza kua elimu hii ya kijinsia inavyoweza kuwafikia kwa wapesi wanajamii na kuwasaidia ni kwa njia ambazo ni rafiki kama vile vikundi vya Sanaa, makongamano, elimu rasmi kama vile mashuleni na vyuoni, kuwaalika wataalamu wa kijinsia kuwapa elimu na ujuzi kwa wanajamii njia hizi zitasaidia kwasababu zitawafikia kwa mda mfupi na kuwaepusha na matukio ya unyanyasaji wakijinsia.

“Kama elimu hii ya kijinsa itaanza tangu mwanzo kabisa kama kwa watoto wadogo na katika ngazi ya familia itasaidia kwa kiasi kikubwa kupeleka ujumbe na kujenga jamii iliyo bora. Pia katika upande wa dini zote mbili ni sahihi kutumia njia hiyo ya kidini kufikisha ujumbe kwa wanajamii.

Kama jamii itapata elimu hii basi itasaidia kuleta kujitambua baina ya wanajamii na kujua nafasia zao katika familia na jamii kiujumla, elimu hii pia itasaidia kujenga kujiamini, kujithamini na kuelewa majukumu ya kila jinsia. Juhudi zote hizi zinawezakana kama tu jamii inayofikishiwa elimu hii inautayari wa kupokea elimu hii na kuifanyia kazi ipasavyo, njia hizi zitasaidia kuipeleka jamii mahali husika.”

 

Mwandishi: Helieth Ngeze

Leave a Comment