×

Mashindano ya Kitaifa ya UCMAS 2023 Kuwajengea Wanafunzi Uwezo wa Hesabu Yatingisha

 

KAMPUNI ya UCMAS inayosimamia Program ya Jumla ya Mfumo wa Hesabu za Akili, kwa mara ya pili leo imefanikisha mashindano yake ya hesabu kwa watoto wa shule mbalimbali za msingi ili kufanikisha dhima yao ya kuwajengea uwezo wa kiakili.

Akizungumza Mkurugenzi wa UCMAS Mili Rughan alisema: Kuhusu UCMAS kwa kifupi naweza kusema kuwa, inasimamia Dhana ya Jumla ya Mfumo wa Hesabu za Akili.

“Ni mbinu ya kipekee na iliyothibitishwa Kisayansi ya kufundisha hesabu ya akili kwa watoto wenye umri wa miaka 4 hadi 13, Kwa kutumia UCMAS, watoto hujifunza jinsi ya kufanya hesabu ngumu za hisabati haraka na kwa usahihi, bila hitaji la kikokotoo au hata kalamu na karatasi.

 

 

“Wanajifunza jinsi ya kutumia akili zao kufanya hesabu kwakutambua kuwa ni ujuzi muhimu ambao utawanufaisha katika maisha yao yote, UCMAS sio tu kuhusu kujifunza hesabu, lakini pia hukusaidia kuboresha kumbukumbu, umakini, ubunifu, na ujuzi wa kutatua matatizo, ambao wote ni ujuzi muhimu huwasaidia watoto katika maisha yao ya kitaaluma na ya kibinafsi.

Kwa upande wa Mgeni rasmi wa mashanidano hayo, Mercy Mchechu, ambaye ni Mkurugenzi na Mmiliki Mwenza wa Shule za Rightway, alisema: Tunaipongeza sana UCMAS kwa kuona umuhimu wa kuja na program ya mafunzo haya ya hesabu, maana kufanya hivi ni njia moja wapo ya kuandaa kizazi kitakachokabiriana na masomo ya hesabu ambayo yamekuwa yakiwashinda wanafunzi wengi,” alisema Mchechu.

Leave a Comment