×

Rais Samia Avunja Bodi ya Shirika la Reli (TRC) na Kutengua Uteuzi wa TGFA

Rais Samia Suluhu Hassan, leo April 9, 2023 ametangaza kuvunja bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) pamoja na kutengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Mhandisi John Nzulule.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa katika hatua nyingine, Rais Samia amemuelekeza Katibu Mkuu Kiongozi kuhakikisha kua makatibu wakuu na watendaji wakuu wote wa taasisi za serikali wanaipitia kwa kina taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kujibu na kuzifanyia kazi kwa haraka hoja zote zinazogusa maeneo yao.

Pia Rais Samia ameelekeza kuwa watendaji wote watakaobainika kuhusika na uzembe au ubadhirifu wachukuliwe hatua za kisheria.

Leave a Comment