
Shirika la Habari la Kuwait News, limemtambulisha mtangazaji wake wa kwanza ambaye ameundwa kwa teknolojia ya Artificial Inteligence (AI), aliyepewa jina la Fedha.
Licha ya kuonekana akifanana kama binadamu wa kawaida kuanzia mwonekano, matamshi na mijongeo ya mwili, Fedha si binadamu halisi bali ni picha jongevu iliyoundwa kwa AI, ikiwa na sifa zote za binadamu.
Abdullah Boftain, Mhariri Mkuu Msaidizi wa Shirika la Kuwait News, ameliambia Shirikala Habari la AFP kwamba wamekuja na ubunifu huo mpya kwa lengo la kuboresha huduma zao za utoaji wa habari.
Katika video iliyorushwa kupitia akaunti ya Twitter ya Kuwait News, Fedha anasikika akijitambulisha kwa lugha ya Kiarabu: “Naitwa Fedha, mtangazaji wa kwanza nchini Kuwait ninayefanya kazi kupitia teknoloji aya Artificial Inteligency katika Shirika la Kuwait News. Ni aina gani ya bahari unazipendelea? Nataka kusikia maoni yako.”
Boftain amesema kwa sasa wanamfundisha Fedha lafudhi ya Kuwait na siku chache zijazo, ataanza kusoma taarifa ya habari runingani.