Mbunge wa Lindi, Viti Maalum kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Maimuna Pathan leo April 12, 2023 amemwaga machozi bungeni wakati akichangia mada kuhusu uharibifu unaofanywa na tembo kwenye mashamba ya wakulima sehemu mbalimbali nchini, ikiwemo Lindi.
Maimuna amesema wananchi wanapoteza maisha kwa kuuliwa na tembo lakini serikali haichukui hatua za haraka kudhibiti maafa hayo, lakini inapotokea tembo ameuawa na wananchi, maafisa wa wanyamapori hufika haraka eneo la tukio na kuanza kuwasumbua wananchi.