×

Yanga Wafunguka Morrison Kuuza Mechi Nigeria dhidi ya Rivers

 

Bernard Morrison.

BAADA ya tetesi kuenea juu ya winga wa Yanga, Bernard Morrison kushindwa kucheza mchezo dhidi ya Rivers kwa tuhuma za kutaka kuihujumu timu hiyo, uongozi wa Yanga umefunguka juu ya sakata hilo na kuweka uwazi mzito.

Morrison licha ya kusafiri na timu kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo kati ya Yanga dhidi ya Rivers hakuwepo katika sehemu ya kikosi kilichoshiriki mchezo huo na kuzua sintofahamu nyingi kwa mashabiki wao.

Jumapili iliyopita, Yanga ilikuwa ugenini Nigeria kucheza mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji wao Rivers na kushinda mabao 2-0.

Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema kuwa wao wenyewe walishitushwa na taarifa za Morrison kutaka kuwahujumu huku wakiweka wazi kuwa taarifa hizo ni za uzushi kwani hazina ukweli wowote na anaamini watu waliofanya hivyo walikuwa wanafanya kwa lengo la kuwatoa mchezoni.

“Tulishangazwa sana na taarifa za watu juu ya mchezaji wetu Bernard Morrison kutaka kutuhujumu, hawa watu bila shaka walitaka kututoa mchezoni kuelekea katika mchezo wetu dhidi ya Rivers, bahati mbaya kwao Yanga hii sio Yanga wanayoifahamu wao.

“Morrison kama kweli alikuwa na mpango wa kutuhujumu sisi tusingempeleka katika mahojiano na Waandishi wa Habari kuelekea katika mchezo wetu, na kwa faida tu ya watu Morrison aliumia kabla ya mchezo na ndio maana hakucheza, alipata majeraha ya goti na hicho ndio chanzo cha yeye kukaa nje na kuwapisha wengine kucheza,” alisema kiongozi huyo.

Stori: Marco Mzumbe

MSANII ALIYEANGUKA CHOONI kwa SHILOLE AFUNGUKA SHISHI KUMUWASHIA MOTO – “DIAMOND ALINIAMBIA NIIMBE”

Leave a Comment