
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka vijana kutumia mitandao ya kijamii vizuri kwani kuna uhuru wa kusema, kutafuta jambo au habari kwani simu inakuwa mkononi mwako kwa hivyo kufanya unalotaka.
Rais Samia ameendelea kuwataka vijana watumie mitandao ya kijamii kwa maendeleo zaidi kwani ina manufaa yake na siyo vinginevyo.
Rais Samia ameyasema hayo leo Mei 13, 2023 aliposhiriki hafla ya utiaji saini Mikataba ya miradi ya kufikisha huduma za mawasiliano ya Simu katika kata 763 nchini katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
