
Kama wewe siyo mkosaji na mkwepa kodi unatoa rushwa ya nini kwa Watumishi wa TRA. Dhana tuliyonayo sasa ni kupunguza physical contacts za Watumishi wetu na Wafanyabiashara kwa kufanya yafuatayo:-
1. Kuimarisha mfumo wetu wa Forodha (TANCIS) uwe wa kisasa ili kuhakikisha unaondoa changamoto chache zilizopo;
2. Kukamilisha Ujenzi wa Mfumo wa Kodi za Ndani (IDRAS);
3. Mifumo yetu hii miwili ikisomana na Wafanyabiashara wakazingatia kusajili Maghala yao ili stock yao iwe monitored na wakitumia ilivyosahihi mashine za EFD, basi tutakuwa hatuna ugomvi nao;
4. Hivyo, malalamiko ya Wafanyabiashara yanakinzana na kufikia malengo haya.
Hapa kinacholeta vurugu ni watu kutaka Uholela v/s kufuata Sheria za Nchi. Nadhani tunaweza kuchangia vizuri zaidi tukifahamu chimbuko la suala hili. Watu wachache wenye maslahi binafsi hawawezi kulazimisha uharamia wa kuvunja sheria. Kama sheria za Kodi zina changamoto wasema zirekebishwe kwa kufuata utaratibu na siyo kugoma!