Wafanyakazi wa Vodacom Wachangia Damu Katika Hospitali ya Rufaa Dodoma
Global Publishers May 15, 2023 0 Comments
SHARE THIS:
WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania, Mei 15, 2023 walifika katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma (General) kwa ajili ya kuchangia damu kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji huduma ya kuongezewa damu katika hospitali hiyo.
Mbali na kuchangia damu, pia wafanyakazi hao walitoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika wodi za mama na mtoto hospitalini hapo.
Afisa Mteknolojia Maabara wa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Renatus Mayunga akiwapa maelezo wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom Tanzania Mkoa wa Dodoma walipofika hapo jana kuchangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa wanaofika kupata matibabu hapo.
Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kati, Joseph Sayi akisaidiwa kutolewa damu na Mteknolojia wa Maabara ya Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Aziza Hamisi. Wafanyakazi wa kampuni hiyo Mkoa wa Dodoma walitembelea hospitalini hapo jana kuchangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa wanaofika kupata matibabu.
Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kati, Joseph Sayi (kulia) akimkabidhi mojawapo ya msaada Bi. Rehema Mustafa aliyelazwa wodi mamba 23 Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kujifungua. Wafanyakazi wa kampuni hiyo walifika hospitalini hapo siku ya jana kukabidhi misaada ya mahitaji mbalimbali katika jengo la mama na mtoto.