×

Picha: Mazishi ya Bernard Membe Yalivyofanyika Kijijini Kwao Rondo

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe, Wakitoa Salamu za Mwisho Kando ya Kaburi la Bernard Membe wakati wa mazishi yake.

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kuongoza mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe yaliyofanyika katika Kijiji cha Rondo, leo Mei 16, 2023.

Jeneza la Bernard Membe, kabla ya kuzikwa kijijini kwao, Rondo.

 

Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete na mkewe, Salma Kikwete ni miongoni mwa waombolezaji waliohudhuria mazishi ya Membe.

Ibada ya mwisho ya marehemu Benard Membe iliyofanyika kijijini kwao, Rondo kabla ya mazishi.

 

Membe alifariki dunia katika Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam Ijumaa ya Mei 12, 2023 baada ya kuugua kwa muda mfupi.

 

Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete na mkwe, Salma Kikwete wakielekea kuweka shada la maua kwenye Kaburi la Bernard Membe wakati wa mazishi yake.

 

Ibada ya mwisho ya marehemu Bernard Membe iliyofanyika kijijini kwao, Rondo kabla ya mazishi.

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe, wakiweka shada la maua kwenye Kaburi la Bernard Membe wakati wa mazishi yake.

 

 

Leave a Comment