×

Auawa na Watoto; Kisa Mchepuko wa Baba Yao

POLISI katika Kaunti ya Kisumu nchini Kenya wanawasaka vijana wawili kwa tuhuma za kumuua mpenzi wa baba yao mzazi, Mercy Akinyi (29) ( pichani) tukio ambalo linadaiwa kufanyika usiku wa Jumatano, Aprili 8, 2020, baada ya kumfuma dada huyo akitoka kwenye nyumba ya baba yao.

 

Inaelezwa kuwa vijana hao walikuwa wakimtuhumu baba yao kuanza mahusiano na mwanamke huyo, na kumtelekeza mama yao mzazi ambaye yupo hospitali katika chumba cha wagonjwa mahtuti (ICU) akipatiwa matibabu kwa muda sasa.

 

Jeshi la polisi limesema kuwa, katika uchunguzi wa awali limebaini kwamba dada huyo (Akinyi), alionekana akinywa pombe na mchepuko wake (baba wa vijana hao) kwenye baa moja ya kienyeji, huko Nanga, Kisumu.

Imeelezwa kwamba walikubaliana kwenda kujivinjari pamoja katika nyumba ya mzee huyo anayejulikana zaidi kwa jina la Mwalimu ambaye aliondoka mapema eneo hilo kwa makubaliano kuwa mchepuko angemfuata nyumbani kwake baadaye kidogo.

 

Akinyi alifika nyumbani hapo, baada kumaliza kujivinjari na baba huyo  aliondoka kwenye himaya ya Mwalimu majira ya saa 5;00 usiku.

Lakini wakati akitoka nje tu aliangukia kwenye mikono ya vijana hao wawili ambao walikuwa wakimsaka kwa muda mrefu kutokana na tuhuma za kutoka kimapenzi na baba yao mzazi.  Walimshambulia kwa mapanga na mawe na huo ndiyo ulikuwa mwisho wa maisha yak.

 

Akinyi amefariki akiwa na ujauzito wa miezi mitatu na mtoto mdogo mwenye umri wa miaka 10.

Leave a Comment