×

Inter Yaweka Rekodi UEFA Yatinga Fainali kwa mara ya Kwanza

INTER Milan imeweka rekodi ya kutinga Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka 13, ikiwa chini ya Kocha Simone Inzaghi.

Juzi Jumanne, Inter iliifunga AC Milan bao 1-0 katika nusu fainali ya pili na kutinga fainali kwa jumla ya mabao 3-0 baada ya mchezo wa kwanza ugenini kushinda 0-2.

Ndani ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mara ya mwisho Inter kucheza fainali ilikuwa mwaka 2010 ambapo ilitwaa taji hilo chini ya Kocha Jose Mourinho ikiifunga Bayern Munich.

Hii itakuwa ni fainali ya sita Inter inacheza ndani ya UEFA ambapo katika fainali tano zilizopita, ilifanikiwa kutwaa mataji matatu mwaka 1964, 1965 na 2010.

Ndani ya mwaka huu wa 2023, Inter imefanikiwa kushinda mechi nne mfululizo mbele ya Milan walipokutana katika michuano tofauti, huku Milan ikishindwa kufunga bao hata moja mbele ya wapinzani wao hao.

Lautaro Martinez ndiye alikuwa shujaa kwa Inter Milan baada ya juzi kufunga bao pekee la ushindi katika mchezo huo na bao lake lilikuwa la 25 msimu huu kwenye michuano hiyo.

Nyota huyo ambaye ni mshindi wa Kombe la Dunia 2022, anaweza kuwa mchezaji wa 10 kushinda taji la UEFA na Kombe la Dunia kwa msimu mmoja.

UNYAMA DAR! MJAMZITO ACHOMWA MOTO na MUMEWE HADI KUFARIKI, ALIKUWA AKIMTAKA MUME AACHE UZINZI…

Leave a Comment