×

Rais wa Zanzibar, Dk. Mwinyi Akutana na Viongozi wa ACT Wazalendo Ikulu

Rais Dk. Mwinyi (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa ACT Wazalendo.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi leo amekutana na Viongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo ambao ni Mwenyekiti, Mhe. Juma Haji Duni, Makamu Mwenyekiti ambaye ni pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe.Othman Masoud na Mhe.Zitto Kabwe.

Pamoja na mambo mengine yanayohusu ustawi wa Zanzibar kisiasa na kijamii Viongozi hao wameafikiana kwamba ipangwe tarehe ya kuzindua rasmi kamati maalum itakayoundwa na wajumbe kutoka vyama vya CCM na ACT-Wazalendo ambavyo ndivyo vilivyounda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, kuanza kujadiliana na baadae kupanga mpango wa utekelezaji wa ripoti ya kikosi kazi kilichoundwa kufuatia Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa uliojadili maeneo mahsusi yanayoihusu Zanzibar.

Kikao hicho kimefanyika Ikulu, Zanzibar

🗓️18 Mei 2023

📍Ikulu , Zanzibar.

 

Leave a Comment