×

Waziri January Makamba: Tanzania Ina Uhakika wa Upatikanaji wa Nishati ya Mafuta

 

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema nchi ina uhakika wa upatikanaji wa nishati ya mafuta kwa muda wa kutosha.

Makamba ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

 

Ameongeza kuwa, uhakika wa upatikanaji wa nishati ya mafuta, una uhusiano wa moja kwa moja kati ya ajira na mapato serikali.

“Aidha, upatikanaji wa nishati safi, ikiwemo vijijini, kunasaidia kulilinda Taifa letu dhidi ya athari za uharibifu wa mazingira,” amesema.

 

 

 

Leave a Comment