×

Wanaotaka Ubunge, Udiwani CCM Kabla ya Muda Sengerema Waonywa

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sengerema, Marco Makoye akiwa kwenye kikao za Baraza la Jumuiya ya Wazazi wa CCM kilichofanyika Wilayani Sengerema Pichana Daniel Makaka

 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Sengerema Marco Makoye amewaonya wanaCCM wanaopita kwenye majimbo kutaka madaraka ya Ubunge na Udiwani kwenye majimbo ya Sengerema na Buchosa kuwa wanapoteza muda chama kiko macho.

Kauli hiyo ameitoa leo Jumatano Juni ,7,2023 kwenye kikao cha Baraza la Jumuiya ya Wazazi wa Chama hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Sengerema.

Amesema kunataarifa za wanaCCM ambao wamepita majimbo kuweka vikao na kuanza kuwahadaa wanachama wa CCM hivyo chama kinawamulika hivyo wanatakiwa kuacha tabia hicho chama kitachukuwa hatua.

Makoye amewataka wanachama hao kuendelea kuunga mkono jitihada za wabunge na Madiwani waliloko madakani wanaotekeleza Ilani ya CCM.

“Sio utarajibu wa chama chetu ambacho ni kikubwa hivyo wanatakiwa kufuata utaratibu wa Chama.na siyo hivyo wanavyofanya , amesema Makoye.

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza hilo Winfrida Chani ameunga mkono kauli ya mwenyekiti wa CCM wa kutoa onyo kwa wanaCCM ambao wanataka madaraka kabla ya muda.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Sengerema Jackson Mazinzi ameitaka Jumuiya hiyo kuwa makini wakati inapotekeleza majukumu yake.

Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Sengerema kimewaonya wanachama wake ambao wameanza kusaka madaraka kabla ya muda kuwa watashughurikiwa.

 

Leave a Comment