×

Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato cha Tano Na Vyuo 2023 haya hapa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Angelah Kairuki amesema wanafunzi 1,878 wakiwemo wasichana 1,097 na wavulana 781 wamepangiwa katika shule za sekondari maalum nane ambazo ni Kilakala, Mzumbe, Ilboru, Kisimiri, Msalato, Kibaha, Tabora Boys na Tabora Girls.

Ameeleza kuwa Wanafunzi  wengine 188,128 waliokidhi vigezo wamechaguliwa na kupangiwa kujiunga na kidato cha tano katika shule mbalimbali nchini pamoja na vyuo vya fani mbalimbali.

Amesema wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka katika shule za serikali, binafsi, watahiniwa wa kujitegemea, waliofanya mtihani chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi.

Leave a Comment