×

Rais Dkt. Samia Ateua Washauri Wake, Lukuvi na Bulembo – Video

Mbunge wa Isimani Iringa William Vangimembe Lukuvi (kushoto) na Mbunge Mstaafu Abdallah Bulembo (kulia).

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Mbunge wa Isimani Iringa William Vangimembe Lukuvi kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii), Lukuvi ni Mbunge wa Jimbo la Isimani, Iringa.

Pia amemteua Mbunge Mstaafu Abdallah Bulembo kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jami).

Amemteua Balozi Rajab Omar Luhwavi kuwa Mshauri wa Rais kwenye Siasa na Uhusiano wa Jamii ambapo Balozi huyu alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji.

Vilevile Rais amemteua Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Waziri Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Haji Omar Kheir kuwa Mshauri wa Rais upande wa Siasa na Uhusiano wa Jamii.

Leave a Comment