
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amependekeza kuanzia mwaka wa Fedha 2023/24 kupunguza Ushuru wa Bidhaa kutoka Tsh. 4,386 kwa lita hadi Tsh. 2,466.45 kwa lita kwenye vinywaji vikali (Ready to Drink) vinavyozalishwa nchini
Amependekeza kutoza Ushuru wa Bidhaa kwa kiwango cha Shilingi 20 kwa kila kilo moja ya Saruji inayotoka nje ya nchi na inayozalishwa nchini, kutoza Ushuru wa 5% kwenye magari yenye CC 1000 hadi 2000 yaliyotokana na ukuaji wa teknolojia na Ushuru wa 10% kwenye magari ya abiria yanayoingizwa nchini yanayozidi umri wa miaka 5
Aidha amependekeza kutoza Ushuru wa Bidhaa kwa kiwango cha 30% kwenye Sigara na bidhaa za aina hiyo zinazotumia mbadala wa Tumbaku inayovutwa kwa kutumia bomba na Sigara za Kielektroniki (Shisha) na bidhaa za aina hiyo