×

Kituo cha Uwekezaji (TIC), Kampuni ya Sukari Kilombero Wasaini Mkataba wa Utekelezaji

Juni 23, 2023, Serikali ilishuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji kati ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na wawekezaji kwa lengo la kukabiliana na uhaba wa bidhaa muhimu nchini.

 

Kampuni ya Sukari Kilombero ilisaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wake wa upanuzi unaotekelezwa mkoani Morogoro ambao unahusisha upanuzi wa mradi wa kilimo cha miwa na kiwanda kwa ajili ya uzalishaji wa sukari.

 

Baada ya kukamilika, mradi huo utakaogharimu dola za Kimarekani 238.5 milioni, utaleta ajira mpya zipatazo 1,404 za moja kwa moja na 15,000 ambazo si za moja kwa moja.

 

Baada ya upanuzi, kampuni itakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 271,000 za sukari na hivyo kupunguza mahitaji ya uagizwaji sukari kutoka nje.

Leave a Comment