×

Beki Kitasa Azuiliwa Simba Kuendelea kubaki Msimu Ujao

Jonas Onyango.

SIMBA imetangaza kuwa beki wao Mkenya, Jonas Onyango, bado mali ya timu hiyo, na ataendelea kuwa mchezaji wao kwa msimu ujao.

Onyango ni kati ya wachezaji wanaotajwa kuondoka hapo, licha ya mkataba wake kubaki mwaka mmoja, huku mara kadhaa ikiripotiwa kwamba ameandika barua ya kusitisha mkataba wake huo.

Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema Onyango bado ataendelea kubaki Simba kwa msimu ujao.

Aliongeza kuwa bado beki huyo anahitajika katika timu hiyo, kutokana na ubora alionao wakati wakijiandaa na michuano ya kimataifa msimu ujao.

“Hicho kinachoendelea na uvumi tu, hakuna barua yoyote tuliyoipokea kutoka kwa Onyango ya kuomba kuondoka.

“Watu wafahamu kuwa Onyango ni mchezaji halali wa Simba ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika msimu ujao,” alisema Ally.

STORI NA WILBERT MOLANDI

ALLY KAMWE AFUNGUKA USAJILI YANGA, UZINDUZI wa JEZI, NAMBA 6 wa YANGA – “FRIJI HALIGANDISHI”

Leave a Comment