×

Rais Agomea Nyongeza Ya Mshahara Wake, “Walimu, Polisi Wanastahili”

Rais wa Kenya, William Ruto.

RAIS wa Kenya, William Ruto amegomea pendekezo la Tume ya mishara ya nchi hiyo (SRC) la nyongeza ya mshahara kutoka TSh 24.8 milioni anaopokea sasa hadi Tsh milioni 28.3 ambalo angeanza kupokea katika mwaka huu wa fedha 2023/2024.

Pia amekataa nyongeza ya mishahara kwa Naibu wake, mawaziri na maofisa wengine wa ngazi za juu serikalini, badala yake ameitaka tume hiyo ya kushughulikia nyongeza ya mishahara ya watumishi wa umma kama vile walimu, askari polisi na watumishi wengine wa ngazi za chini. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Ruto amesema hayo leo tarehe 1 Julai 2023 katika uzinduzi wa huduma za serikali katika jumba la KICC nchini humo.

Ruto amesema wanaohitaji nyongeza ya mishahara ni maafisa wa polisi, walimu na baadhi ya wafanyakazi wengine wa serikali.

Kwa mujibu wa rais Ruto, maafisa wa ulinzi chini ya kikosi cha Jeshi, maarufu KDF, pia watapewa nyongeza kwenye mishahara yao.

Nyongeza hiyo ambayo itafanywa na tume ya mishahara nchini Kenya itakuwa ya kati ya asilimia 7-10.

Aidha, Rais Ruto amesema yeye, naibu wake Rigathi Gachagua, Kiongozi wa Mawaziri Musalia Mudavadi na maafisa wengine wakuu hawatapokea nyongeza hiyo.

Hayo yanajiri wakati ambapo Wakenya wengi wanalia kuhusu kuongezeka kwa gharama ya maisha haswa baada ya mswada wa fedha 2023 kupitishwa

Tume ya mishahara ya nchi hiyo (SRC), ililuwa imependekeza Rais kupokea KSh 1.65 milioni (TSh. 28.3 milioni) kuanzia Julai 1, 2024.

Naibu Rais angepata KSh 1,367,438 (Tsh. 23.4 milioni), kutoka KSh 1,227,188 (Tsh 21 milioni) na ongezeko lingine hadi KSh 1.4 milioni (Tsh. 24 milioni) Julai 1, 2024, ambayo ni ongezeko la 14%.

Katibu Mkuu Mkuu Musalia Mudavadi na mawaziri wengine wangepokea KSh 1,056,000, kutoka KSh 924,000, kuanzia Julai 1, 2023.

YANGA KUMENOGA! WASAINI DILI LINGINE KUBWA, WANACHAMA WAPEWA SHAVU, INJINIA HERSI AFUNGUKA…

Leave a Comment