×

RC Chalamila Amuapisha DC Mpya Temeke Mobhare Holmes Matinyi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila leo Julai 4, 2023 amemuapisha Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mobhare Holmes Matinyi kufuatia uteuzi uliofanywa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan

Hafla ya Uapisho huo imefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkoa huo Ilala Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Sekretarieti na Wilaya za Mkoa huo wakiongozwa na katibu Tawala wa Mkoa Bi Rehema Madenge

RC Chalamila amemtakia majukumu mema katika kuwahudumia wananchi wa Wilaya ya Temeke huku akitoa rai kwa Viongozi wa Manispaa na Wilaya kumpa ushirikiano kiongozi huyo.

ROSTAM AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI “ULIMI ULITELEZA”…

Leave a Comment