×

Makampuni Na Taasisi Arusha Zafurahishwa Na Huduma Ya NBC Connect

Mkuu wa kitengo cha huduma za kibenki kwa makampuni na taasisi wa NBC James Metairon akielezea namna huduma ya NBC Connect inavyoweza kurahisisha ufanyaji wa miamala kidigitali kwa wateja wa benki hiyo katika Hafla ya Uzinduzi wa huduma hiyo iliyofanyika jijini Arusha.

Arusha Julai 5, 2023: Taasisi na makampuni wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) mkoani Arusha, wameipongeza benki hiyo kwa kuwapelekea huduma ya malipo kidigitali inayojulikana kama NBC Connect inayosaidia kuokoa muda na kuongeza ufanisi.

Baadhi ya wateja walioalikwa katika uzinduzi wa huduma hiyo mkoani Arusha walisema NBC connect itaziwezesha taasisi zao kufanya malipo kwa njia ya usalama na bila kulazimika kufika kwenye matawi ya benki jambo ambalo litasaidia kuokoa muda.

NBC Connect, ni huduma ya kisasa ya kidigitali kwa makampuni na taasisi mbalimbali, ambayo huwezesha huduma salama za kibenki kufanyika sehemu yoyote, muda wowote kwa njia ya mtandao.

Joseph Buko kutoka kampuni ya Rhotia Valley alisema pamoja na kusaidia kuokoa muda, mfumo huo wa malipo kidigitali utaongeza ufanisi kwakuwa unaruhusu kufanya miamala mingi kwa wakati mmoja na kwa ufanisi.

 Mgeni rasmi katika uzinduzi wa huduma ya NBC Connect, Naibu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha David Lyamongi (watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki ya NBC na baadhi ya wateja walioalikwa kwenye uzinduzi wa huduma ya NBC Connect inayowezesha kufanya miamala kwa urahisi kwa njia ya kidigitali. Hafla hiyo imefanyika jijini Arusha.

“Tunaishukuru benki ya NBC kwa kutulea huduma hii nzuri. Kulingana na mawasilisho yao kwetu, ni wazi kuwa itatusaidia sana kuokoa muda na muhimu zaidi, kuongeza ufanisi katika shughuli zetu za kila siku,” alisema.

Mteja mwingine aliyejitambulisha kama Yusuph Zege kutoka University of Arusha aliishukuru benki ya NBC kwa kuja na huduma hiyo ya kibunifu na kuongeza kuwa inaonyesha namna ambavyo benki hiyo inawafikiria na kuwajali wateja wake ambao ni taasisi binafsi na za serikali.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa wateja wakubwa Bw. James Metairon alisema, “Tunafuraha kutambulisha NBC Connect kwa wakazi wa  Arusha. Mfumo huu wa kibenki wa kidigitali ni uthibitisho wa dhamira ya kuwapatia wateja wetu huduma bora za kibenki ambazo ni rahisi, salama na kukidhi mahitaji yao. NBC Connect itawawezesha wateja wetu wenye makampuni na taasisi mbalimbali kufanya huduma za kibenki popote pale, wakati wowote, na kufurahia huduma hizo bila matatizo.”

Pamoja na huduma rahisi na za kisasa, NBC Connect itatoa usaidizi binafsi kwa wateja kupitia kituo chake cha huduma kwa wateja ambapo mameneja wetu wanapatikana ili kuwasaidia wateja kulingana na mahitaji yao na kutoa mwongozo wa jinsi ya kutumia huduma hilo kwa ufanisi.

Naibu Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha David Lyamongi,akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya NBC Connect inayowezesha kufanya miamala kwa urahisi kwa njia ya kidigitali. Hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo ilifanyika jijini Arusha.

“Tunawaalika wateja wetu wote wa Arusha wajionee urahisi na usalama wa NBC Connect. Ni huduma ambayo inaleta mapinduzi mapya kwenye namna ambavyo huduma za kibenki zinatolewa. Tuna uhakika kuwa wateja wetu watafaidika nayo kwa kiasi kikubwa, “aliongeza.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Katibu msaidizi Tawala Mkoa wa Arusha Ndugu David Lyamongi aliishukuru Benki ya NBC kwa ubunifu wao mzuri na kuwahimiza wateja kutumia mfumo huo mpya wa kibenki ili kurahisisha shughuli zao za kibenki.

Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi wa huduma ya NBC Connect inayowezesha kufanya miamala kwa urahisi kwa njia ya kidigitali. Hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo ilifanyika jijini Arusha.

“Uzinduzi wa NBC Connect Arusha unawakilisha mpango mkakati wa upanuzi wa benki ya NBC ili kufikia taasisi mbalimbali na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

Benki ya NBC inasifika kwa dhamira yake ya kuwajibika kwa jamii, ikiwa ni pamoja na kusaidia jamii kupitia mipango mbalimbali, kama vile Mbio za Kimataifa za NBC Dodoma Marathon zinazohamasisha matibabu ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake, msaada wa afya ya uzazi kupitia kliniki zinazotembea, programu za elimu ya kifedha, uwezeshaji wa vijana. Kupitia udhamini wa Ligi Kuu ya NBC, hakika napongeza juhudi hizi zinazofanywa na NBC” alisema.

Kuhusu Benki ya NBC:

Benkiya NBC ni taasisi ya kifedha inayoongoza nchini Tanzania inayotoa bidhaa na huduma mbalimbali za kibenki kwa watu binafsi, wafanyabiashara na jamii. Kwa kujitolea kwa dhati kwenye suala la huduma kwa wateja, uvumbuzi, na uwajibikaji wa kijamii, NBC Connect inalenga kuwa mshirika wa benki anayeaminika kwa watu binafsi na biashara Tanzania nzima.

Leave a Comment