×

Beki Mpya Mcameroon Atuma Ujumbe Simba

Fandoh Che Malone

RASMI sasa beki wa kati wa Cotton Sports ya nchini Cameroon, Fandoh Che Malone anakuja Simba ni baada ya kuwatumia ujumbe viongozi wa timu hiyo kuwa jezi namba 6 asipewe mchezaji yeyote yule kwani anakuja kuivaa yeye.

Jezi hiyo namba 6 ilikuwa ikivaliwa na Mnigeria, Victor Akpan katika msimu uliopita ambaye ameshapewa ‘Thank You’ lakini kabla yake alivaa Muivory Coast, Pascal Segre Wawa.

Championi Jumatano, liliripoti taarifa za Simba kufikia makubaliano mazuri na beki huyo kwa kumsajili baada ya kuisaka saini yake kwa muda mrefu.

Gazeti hili limepata taarifa kutoka kwa uongozi wa timu hiyo, kuwa jezi namba 6 isiguswe na mchezaji yeyote, kwani tayari ina mwenyewe ambaye ni Che Malone.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa uongozi tayari umetoa taarifa kwa benchi la ufundi la timu hiyo, jezi namba 6 isivaliwe na mchezaji yeyote yule mpya au wa zamani, kwani tayari imewahiwa.

“Che Malone amethibitisha kuwa rasmi anakuja Simba mara baada  ya dili kukamilika juzi baada ya mvutano kati ya uongozi wa Cotton Sports na Simba katika dau la usajili.

“Jezi hiyo ndio atakayoivaa atakapotambulisha hadi katika msimu ujao ambayo ilikuwa  ikivaliwa na Akpan ambaye hatakuwa sehemu ya wachezaji wetu msimu ujao,” alisema mtoa taarifa huyo.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa timu hiyo, Ahmed Ally alizungumzia hilo kwa kusema kuwa: “Usajili wetu umekamilika kwa asilimia 80, kilichobakia kuanza kutambulisha wachezaji hao wapya.”

STORI NA WILBERT MOLANDI

RAIS SAMIA AZINDUA JEZI MPYA za YANGA AKIWA MALAWI, AKABIDHIWA YAKE MOJA na RAIS wa MALAWI MOJA…

Leave a Comment