×

Mwanasheria Wa Yanga Aula FIFA Kwa Miaka Mitatu

Mkurugenzi wa Sheria wa klabu ya Yanga Adv Simon Patrick.

Baraza Kuu la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limemchagua Mkurugenzi wa Sheria wa klabu ya Yanga Adv Simon Patrick kwenye jopo la Wanasheria watakaoisaidia FIFA kwenye masuala ya kisheria kwa wachezaji.

Adv Simon Patrick (35) ni Mtanzania pekee kwenye jopo hilo la Wanasheria 21 kutoka sehemu mbalimbali Duniani waliochaguliwa na FIFA na atahudumu kwenye nafasi hiyo kwa miaka mitatu.

Leave a Comment