
Mwigizaji wa Nollywood, Nchini Nigeria, Regina Daniels, ameelezea furaha yake baada ya kualikwa kwenye mwaliko maalum kwenye nyumba ya Seneti na mumewe, Bilionea Ned Nwoko.
Chinedu Nwoko (anayejulikana pia kama Ned Nwoko) ambaye alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa Useneta katika Wilaya ya Delta Kaskazini, Jimbo la Delta, ameanza rasmi jukumu lake katika Ikulu ya Seneti huko Abuja.

Katika ukurasa wake wa Instagram, alielezea heshima hiyo kwa kualikwa kwenye mwaliko maalum na mumewe kushuhudia ofisi yake mpya aliyotengewa.
“Nina furaha Sana. Nilialikwa katika nyumba ya seneti na mume wangu kuona nafasi yake mpya ya ofisi,” alichapisha.