×

Washindi Watatu Waliobahatika Kuondoka Na Pikipiki Mpya Waishukuru “Jaza Ushinde Tena Na Engen”

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vivo Energy Tanzania, Khady Sene (kulia) akimkabidhi funguo mshindi wa promosheni ya Jaza Ushinde Tena na Engen, Michael Kida mkazi wa Kipinguni Gongolamboto aliyejishindia pikipiki mpya baada ya kushiriki kujaza mafuta kwenye vituo vya Engen na kuingia kwenye droo hiyo, makabidhiano hayo yalifanyika Kipunguni jijini Dar es salaam. Wengine wapili kulia Msimamizi wa Kituo cha Kipunguni Muslim Baruani na kushoto ni Meneja wa Mauzo ya Rejareja Vivo Energy Tanzania, Adams Ouedrago.

Dar es Salaam, Julai 2023: Vivo Energy Tanzania imehitimisha msimu wa pili wa promosheni yake ya kitaifa ya “Jaza Ushinde Tena na Engen”. Promosheni hiyo iliwapa wateja fursa ya kuingia kwenye droo ya bahati nasibu kila mara wanapojaza mafuta ya  kiasi cha TZS12,000 kwenye pikipiki na bajaji, TZS60,000 kwenye magari madogo, na TZS120,000 kwenye mabasi na malori.

Zawadi zilizokuwa zikishindaniwa ni pamoja na, vocha za chakula zenye thamani ya TZS100,000 na  vocha za manunuzi zenye thamani ya TZS 100,000 kwenye maduka ya Engen, simu janja, friji, TV na Bodaboda kama zawadi kuu.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vivo Energy Tanzania, Khady Sene (watatu kulia) akimkabidhi Runinga mshindi wa promosheni ya Jaza Ushinde Tena na Engen, Gaston Beatus mkazi wa Bunju jijini Dar es salaam aliyejishindia zawadi hiyo baada ya kushiriki kujaza mafuta kwenye vituo vya Engen na kuingia kwenye droo.

Michael Kida na washindi wengine Finias Boniface na Hatibu Kusaga wa mikoani ambao bado hawajakabidhiwa zawadi zao, Kida  aliondoka na ushindi wa pikipiki mpya kabisa. Gaston Beatus, Fikiri Mtimbuka na Francis David waliondoka na runinga janja za inchi 43, na Edward Mria, Alphan Hassan na Said Mambongo walibeba friji mpya pamoja na washindi wengine wa simu janja, vocha za chakula na vocha za ununuzi. Hii inafanya jumla ya washindi 18 wakati wa kampeni hii.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Vivo Energy Tanzania, Grace Kijo akizungumza wakati hafla ya promosheni ya Jaza Ushinde Tena na Engen.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Vivo Energy Tanzania, Khady Sene,  aliwashukuru wateja kwa kuchagua vituo vya Engen na kuahidi kwamba kampuni hii itaendelea kutoa bidhaa na huduma zilizobora sambamba na kueneza huduma kote nchini, mpaka sasa tuna vituo 41 na tutaendelea kuviongeza kuhakikisha kwamba watanzania wengi wanafurahia huduma zetu.

 

Mmoja wa washindi watatu wa pikipiki, Michael Kida alisema, ‘Napenda kuwahimiza wateja ambao wana shaka na mashindano, kuchukua nafasi kwa sababu mambo mazuri hutokea – siku zote nilitaka kuwa na chanzo cha ziada cha mapato na leo nimekipata, shukrani kwa Engen, kwa kuniwezesha  kufanya hili.’

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vivo Energy Tanzania, Khady Sene (watatu kulia) akimkabidhi Friji na shopping vocha mshindi wa promosheni ya Jaza Ushinde Tena na Engen, Edward Peter Mria mkazi wa Tabata Kinyerezi jijini Dar es salaam aliyejishindia zawadi hiyo baada ya kushiriki kujaza mafuta kwenye vituo vya Engen na kuingia kwenye droo.

Grace Kijo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Vivo Energy Tanzania alisema kuwa kampeni ya “Jaza Ushinde Tena na Engen” ni mwanzo tu wa kampeni nyingi za kusisimua tulizoziandaa, hivyo wateja wetu wanapaswa kutarajia zaidi kila wakati kwa sababu  kwetu sisi wewe ni namba moja, kila mara huwa tunatengeneza bidhaa tofauti tofauti kwa maslahi ya mteja.

Leave a Comment