×

Yanga Yathibitisha Kumsajili Mlinzi wa Kulia Kouassi Attohoula Yao

Kouassi Attohoula Yao

Klabu ya Yanga imethibitisha kumsajili mlinzi wa kulia Kouassi Attohoula Yao kwa uhamisho huru baada ya mkataba wake na klabu ya Asec Mimosas ya Ivory Coast kufikia ukomo.

Yao (26) raia wa Ivory Coast amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Young Africans SC mpaka 2024.

Ujio wa beki huyo huenda safari ikamkuta Djuma ambaye hivi karibuni alikuwepo katika mgogoro na uongozi wake akiomba avunjiwe mkataba wa mwaka mmoja ambao ameubakisha Yanga.

“Utambulisho wa Attohoula ndani ya Yanga utakwenda sambamba na ule wa Zaungrana, kwani ni kati ya wachezaji tuliowasajili kwa ajili ya msimu ujao baada ya kufikia muafaka mzuri na menejimenti ya wachezaji hao.

“Wachezaji hao wote ni mapendekezo ya benchi la ufundi la msimu uliopita ambao walipendekeza beki Djuma aachwe na Attohoula asajiliwe kwa ajili ya kuiboresha safu ya ulinzi.

Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said, hivi karibuni alizungumzia hilo la usajili wa wachezaji wa kigeni kwa kusema: “Kama uongozi hivi sasa tumebadili mfumo wa usajili, usajili wetu wa wachezaji wa kigeni tunaufanya nje ya nchi kwa kumsajili huko nyumbani kwao, akija hapa nchini ni kwa ajili ya utambulisho pekee.

“Tunachokwenda kukifanya msimu ujao ni kuongeza nguvu kidogo tu kwenye mahitaji muhimu, niseme tu tunarudi tukiwa imara zaidi ya ilivyokuwa msimu uliopita,” alisema Hersi.

Leave a Comment