×

Mpishi Alamba Mil 1 Ya “Tigo Chawote” ,Washindi Takribani Elfu 9 nchi Nzima

Meneja Wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi Mary Rutha kushoto akimkabidhi mfano wa hundi Saada Omary.

Saada Omary Mfanyabiashara ya Upishi, Mkazi wa Ilala Jijini Dar Es Salaam ni miongoni mwa washindi wa Milioni Moja,  Kampeni ya Tigo CHA WOTE wiki ya Nne ambapo hadi sasa Tigo wameshatoa Fedha Taslim na zawadi mbalimbali kwa Washindi Takribani 9000 ( Elfu Tisa)  Nchi Nzima tangu kampeni hii izinduliwe.

Tausi Makoba naye akionesha mfano wa hundi baada ya kukabidhiwa mzigo wake kupitia Tigo Pesa.

Akizungumza Leo Julai 21, 2023. Wakati wa Kuwakabidhi Mfano wa Hundi Baadhi ya Washindi wa Milioni Moja Moja wiki ya nne waliobahatika kufika Tigo Makao Makuu, Meneja Wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi Mary Rutha amesema kuwa hadi sasa ikiwa ni wiki Nne tu tangu Kampeni iyo izinduliwe wameshapatikana washindi Takribani 9000  kutoka maeneo mbalimbali nchini.

” Leo tunayo furaha kubwa kuwa na baadhi ya washindi wa Wiki ya Nne wa Kampeni  ya TIGO CHA WOTE ambao hawa ni washindi wa Milioni Moja Moja kila mmoja, Lakini niwakumbushe Watanzania kwamba kila siku CHA WOTE inatoa zawadi ikiwemo pesa taslimu hadi Milioni Moja kwa washindi 320 kila siku , kuibuka mshindi ni rahisi tu unachotakiwa ni kufanya miamala na Tigo Pesa kama Kutumia Lipa Kwa Simu , Kununua Vifurushi , Kulipia Bili kwa Tigo Pesa , n.k kwa kufanya ivyo nawewe siku si nyingi utakua miongoni mwa Washindi wa Kampeni hii ya CHA WOTE “.  ” Alisema Bi. Mary Rutha.

Leave a Comment