×

Waziri Wa Canada Atangaza Neema Kwa Sekta Ya Afya Na Elimu Nchini

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada anayeshughulikia Maendeleo ya Kiuchumi ya Pasific, Harjit Sajjan.

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada anayeshughulikia Maendeleo ya Kiuchumi ya Pasific, Mhe. Harjit Sajjan Julai 20, 2023 akiwa jijini Dodoma kwa nyakati tofauti ametangaza msaada wa Dola za Canada milioni 50 kusaidia maeneo mbalimbali kwenye sekta ya elimu na milioni zingine 105 kusaidia sekta ya afya.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu (kulia) akiongea jambo na Waziri Harjit.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Waziri Harjit ameeleza kuwa licha ya Canada kuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia na Tanzania, Serikali ya nchi hiyo inatambua kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha mazingira ya elimu na upatikanaji wa huduma za afya kwa watu wake. Hivyo Canada imeona ni vyema iunge mkono juhudi hizo ili kuendelea kuboresha maeno hayo kwa maendeleo ya Taifa na watu wake.

 

Akiwa jijini Dodoma kwa nyakati tofauti Waziri Harjit alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu (Mb). Vilevile Waziri Harjit alipata fursa ya kutembelea na kujionea utekelezaji na ufanisi wa programu mbalimbali zinazofadhiliwa na Serikali ya Canada katika Hospitali ya Makole.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda (Mb)

 

CHOTA MAPENE ndiyo mchongo mpya town! Kwa shilingi 1,000 tu, yaani BUKU unajichotea mapene kibao au kupata nafasi ya kujishindia ZAWADI MBALIMBALI KILA SIKU, KILA WIKI kupitia Global TV, Global Radio na mitandao ya kijamii! ======================== Ingia kwenye simu yako📲, sehemu ya kufanyia malipo, andika namba ya kampuni 553111, kumbukumbu namba 255 au andika neno GLOBAL. Weka kiasi cha shilingi 1,000, weka namba yako ya siri, thibitisha na tuma.👍 PEASA UTATUMIWA MOJA KWA MOJA KWENYE SIMU YAKO!🤝👍💰 ============================================================ ⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI? ⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 713 750910), ( +255 783453136) ⚫️ Email: [email protected]

 

Leave a Comment