
Dar es Salaam, Julai 2023:Kampuni inayoongoza kwa huduma za usafiri kwa mtandao barani Afrika Bolt, leo imezindua kitengo cha Driver Selfie Check kama sehemu ya juhudi zake zinazoendelea za kuweka kipaumbele kwa usalama na kupambana na uigaji holela wa madereva wanaotumia akaunti hiyo kwenye mtandao.
Kitengo hiki kipya kitahitaji madereva kujipiga picha wanapoingia mtandaoni, na hivyo kuhakikisha uthibitisho wao wa utambulisho na kuoanisha maelezo yaliyotolewa katika mfumo wa program na picha zao walizotumia. Kwa kutekeleza kitengo hiki, Bolt inalenga kudumisha usalama wa jumla wa watumiaji wake kwenye mtandao.
Kwa miaka mingi, Bolt imeanzisha vitengo vya ziada kwenye jukwaa lake ili kuimarisha usalama na ustawi wa madereva, waendesha bodaboda na abiria wakati wa safari za Bolt. Driver Selfie Check ni kitengo kilichoongezwa, hutoa usalama ulioimarishwa kwa watumiaji kwenye jukwaa la Bolt kwani uhakiki na udhibiti wa madereva ili kuepuka kesi za uigaji pia huwazuia kushirikisha akaunti zao kwa wengine.
Mara tu dereva anapoingia mtandaoni, atashawishiwa kupiga selfie ili kuthibitisha utambulisho wake. Ikiwa selfie hailingani na maelezo ya dereva yaliyotolewa hapo awali, dereva atazuiwa kutoa huduma zake kwenye mtandao hadi maelezo yake yatakapothibitishwa.
“Kwa Bolt, usalama wa abiria na madereva wetu utabaki kuwa sehemu yetu kuu. Tumejitolea kuendeleza uvumbuzi na kutoa vitengo vya kipekee vya usalama. Dhamira yetu inahusu kutoa huduma za bei na fuu, za ubora wa juu na salama.
Tunakuletea kitengo kipya cha ukaguzi wa madereva Driver Selfie Check kulingana na dhamira hii italenga kuboresha hali ya usalama kwa madereva na watumiaji wote kwenye mfumo wetu. Kwa kuzuia madereva vishoka na kuimarisha usalama zaidi wa waendeshaji, kitengo hiki kitaimarisha uimara wa huduma zetu kwa wasafiri. Alisema Charles Matondane, Meneja Mkazi Bolt Tanzania.
Programu ya Bolt pia ina vitengo vingine vya usalama ikiwa ni pamoja na:
- Kitengo cha uthibitishaji wa dereva na gari kwenye program ambacho huruhusu abiria kuangalia na kuthibitisha kuwa dereva na gari linalowachagua, ni sawa na linaloonyeshwa kwenye mtandao.
- Kitengo cha “Driver trip-sharing” hiki ushirikisha safari za madereva kwa kutoa usalama ulioimarishwa kwa kuwaruhusu kushirikisha safari zao za moja kwa moja na mtu mwingine, ambaye atakuwa na fursa ya kufuata safari na eneo katika muda halisi. Pia hufuatiliwa na kusimamiwa kwa wakati halisi na Bolt katika safari yote.
- Kitengo cha ETA kwenye program hii inawawezesha madereva kutoa maelezo yao ya safari ya moja kwa moja na nambari za mawasiliano ya dharura, na hivyo kuimarisha usalama katika safari yao yote.
- Kitufe cha dharura cha SOS ambacho kinaweza kutumika kutahadharisha na kutafuta usaidizi wa usalama au matibabu wakati wowote wa safari ambapo dereva, abiria, au mtumiaji mwingine wa barabara yuko hatarini.
- Vitengo vya alama za abiria na madereva ambavyo pia huruhusu madereva na abiria kukadiria kila baada ya safari. Kitengo hiki hufuatilia namna kama ilivyo kadiriwa na madereva au abiria, nahuruhusu Bolt kuonya au kuzuia mtu yeyote mwenye tabia isiyokubalika. Ukadiriaji huzingatiwa kwa uangalifu na hushughulikia hali ambapo ukadiriaji huo ni wa chini au tukio limeripotiwa.
Bolt itaendeleza vitengo na utendaji unaoboresha mfumo wa usalama wa program zake, kupitia uvumbuzi na uwekezaji unaoendelea, kampuni inajitahidi kutoa matumizi bora zaidi kwa watumiaji wetu, na kuhakikisha usalama wao unapewa kipaumbele kila wakati.
Kuhusu Bolt:
Bolt ni programu bora zaidi ya Ulaya iliyo na dhamira ya kufanya usafiri wa mijini kuwa nafuu zaidi, salama na endelevu.
Bolt ina wateja milioni 100 katika nchi 45 na zaidi ya miji 500 kote Ulaya na Afrika. Kampuni inalenga kuharakisha mabadiliko kutoka kwenye magari yanayomilikiwa hadi usafirishaji wa pamoja, ikitoa njia mbadala bora kwa kila hali ya utumiaji, ikiwa ni pamoja na kukodisha gari, magari shirikishi na pikipiki, na usambazaji wa vyakula na mboga.