
Makamu Mwenyikiti wa Chama cha Mapinduzi Bara Ndugu Abdulrahman Kinana ameongoza harambee ya uchangiaji wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu.
Kinana ambaye yeye ndio mlezi wa Mkoa huo katika harambee hio alikua mgeni rasmi na kiasi cha zaidi ya Milioni Mia tatu sabini na tano na laki sita (TZS 375,600,000) zilipatikana.

Harambee hiyo umefanyika Jana usiku katika ukumbi wa Bariadi Cofference Centra ulioko mjini Bariadi, ambapo hafla hiyo ilihudhuliwa na Wadau mbalimbali wakiwemo viongozi na wafanyabishara kutoka ndani ya Mkoa huo.
Wakati anafunga harambee hio Ndugu Kinana alisema anayo furaha kualikwa kuwa mgeni rasmi katika harambee hio lakini pia amewaasa wajumbe wa kamati ya ujenzi na viongozi kuwa fedha zizilizochangiwa ni kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za CCM hivyo wasije kubadilisha matumizi ya fedha hizo na ujenzi uanze mara moja.
Kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana amewashukuru na kuwapongeza wote walioshiriki katika harambee hiyo.
