×

Infinix Yaibuka Kifua Mbele Tuzo Za Kimataifa

Kampuni ya simu za mkononi yenye makao makuu yake nchini Hong Kong yaendelea kupasua anga kimataifa hii ni kufuatia ushindi wa Tuzo ya usanifu ya muundo wa bidhaa/vyombo vya habari na electroniki vya nyumbani kwa mwaka huu wa 2023.

Infinix imejipatia Tuzo hiyo kupitia Infinix NOTE 30, muundo wa simu hii umeipaheshima kubwa kampuni hiyo katika Tuzo hizi za Usanifu wa Ndani, Usanifu wa Mandhari, Usanifu waPicha na Muundo wa Bidhaa ambao hutunukia wabunifu bora zaidi duniani kote kila Mwaka. https://dna.paris/winner/zoom.php?eid=71-90434-23)

“Hii ni heshima kubwa kwetu kama kampuni ambayo inakuwa kwa kasi kubwa inayotokana na uzalishaji wa bidhaa zenye teknolojia ya hali ya juu kwa gharama nafuu,” imeeleza kampuni hiyo”.

Tanzania ni moja ya nchi ambayo inanufaika vyema na bidhaa za kampuni hiyo, imekuwa na mchango mkubwa katika kufanya teknolojia ya mawasiliano kupitia njia ya simu kuenea kwa wepesi.                                                                       

Hii siyo maraya kwanza kwa kampuni hii kushinda tuzo hizo za kimataifa mwaka 2021 pia ilitwaa tuzo ya bidhaa yenye nidhamu Infinix ZERO 8 katika kitengo cha mawasiliano huko barani Asia.

Tutegemee makubwa kutoka kwao kasi yao katika uzalishaji wa simu zenye teknolojia ya hali ya juu si ya kubeza, Hongera nyingi sana kwa ushindi huu na katika kukuza teknolojia ya mawasiliano kupitia njia ya simu.

Leave a Comment