×

Ruzuku ya mbolea yawatia moyo wakulima


Hatua ya Serikali kutoa ruzuku ya mbolea kwa Wakulima imeonesha matokeo chanya kwenye uzalishaji wa mazao ya kilimo nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alipomkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuzungumza na wananchi tarehe 8 Agosti 2023 kwenye kilele cha Maonesho ya Kimataifa ya Nane Nane, jijini Mbeya.

Waziri Bashe amesema eneo la uzalishaji kabla ya ruzuku ya mbolea lilikuwa lilikiwa ekari 10,440,000 mwaka 2021/2022 hadi kufikia hekta 11,137,874.

Ameongeza kuwa matumizi ya mbolea yameongezeka kutoka hekta 363,599 mwaka 2021/2922 hadi tani 580,529 5085,590 mwaka 2022/2023

Aidha, uzalishaji wa chakula umeongezeka kutoka tani. 17,148,290 mwaka 2021/2022 hadi tani 20,42,014 mwaka 2022/2023 sawa na ongezeko la tani 3,000,000.

Leave a Comment