×

Sopu, Prince Dube Waongezewa Makali Kuitungua Yanga Mkwakwani, Tanga

Abdul Suleiman ‘Sopu’

WAKIWA wanajiandaa kuikabili Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii, mastaa wa Azam FC, Prince Dube na Abdul Suleiman ‘Sopu’ wameongezewa makali kwa ajili ya kumtungua kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra.

Azam FC ilikuwa Tunisia kwa kambi ya muda wa takribani wiki tatu kuelekea msimu wa 2023/24 na tayari wamerejea Dar kuendelea na maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo utakaochezwa Agosti 9, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Miongoni mwa mastaa wa Azam FC ambao wanatarajiwa kucheza mechi hiyo ni Sopu aliyemtungua Diarra mabao mawili walipokutana katika Ligi Kuu Bara 2022/23.

Mbali na Sopu, yupo Prince Dube na Idris Mbombo ambao ni washambuliaji, huku Yannick Bangala ambaye ni kiraka akiwa pamoja na Feisal Salum waliokuwa ndani ya Yanga, wamehamia Azam.

Prince Dube

Kocha Mkuu wa Azam FC, Youssouph Dabo, amesema: “Tunaendelea na mazoezi kwa ajili ya kuimarisha kikosi ikiwa ni pamoja na eneo la ushambuliaji ili kupambana na wapinzani wetu, tunatambua kwamba kuna ugumu ila tunajitahidi.”

Mshindi wa mchezo huo, atacheza fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya mshindi kati ya Simba dhidi ya Singida Fountain Gate ambao wenyewe watacheza Agosti 10, mwaka huu, uwanjani hapo. Fainali ni Agosti 13, mwaka huu.

NA LUNYAMADZO MLYUKA NA JOEL THOMAS

HARMONIZE AMPA MAKAVU DIAMOND – ”ASIWADANGANYE, SITAKUWEPO MTWARA, LENGO AJAZE KWETU ANICHAMBE”

Leave a Comment